HAWA WA NITAREJEA YA DIAMOND APOTEZWA NA UNYWAJI WA GONGO

HAWA WA NITAREJEA YA DIAMOND APOTEZWA NA UNYWAJI WA GONGO




INASIKITISHA! Mwanadada mwenye sauti ya kipekee, aliyetamba baada ya kushirikishwa na Diamond Platnumz kwenye wimbo wa Nitarejea, Hawa, ametopea kwenye unywaji wa pombe kali aina ya gongo, kiasi cha kumfanya apoteze mwelekeo maishani mwake.

Amesema kilichomfanya awe mlevi kiasi hicho, ni baada ya mwanaume aliyefunga naye ndoa mwaka juzi, kuondoka na kumuacha bila mawasiliano yoyote kwa muda wa miaka miwili hadi sasa, jambo lililomfanya awe na ‘stress’ nyingi.

Hawa ambaye amedhoofika sana mwili wake na kumfanya kuwa na mwonekano kama mtoto mdogo, akiwa amekondeana sana, amesema awali alikuwa akinywa pombe kali kama Konyagi na viroba lakini baada ya viroba kufungiwa, aliamua kuhamia kwenye gongo.

Amewaomba wadau na mashabiki wake wamsaidie kwani anatamani kuwa sawa na kurudi kwenye hali yake kama zamani kwa sababu anaamini ana kipaji kikubwa ambacho hataki kipotee bure.

Post a Comment

0 Comments