Mabingwa wa kihistoria wa Ligi Kuu Tanzania Bara klabu ya Yanga imefanikiwa kumsajili kiungo wa Mbeya City, Raphael Daud kwa mkataba wa miaka miwili.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/07/20431762_885471001619142_4505273589191357819_n.jpg)
Mchezaji, Raphael Daud
Daud anatarajiwa kujiunga leo katika mazoezi ya klabu hiyo ambayo imeweka kambi yake mjini Morogoro.
![](https://bongo5.com/wp-content/uploads/2017/07/rafael-daudi-mbeya-city_6dpjqizjziip1bklbhn95m93i.png)
Yanga imemsajili Daud kwa ajili ya kuimarisha eneo lao la kiungo ambalo limekuwa na mapungufu makubwa hasa baada ya kumkosa, Haruna Niyonzima kwaajili ya msimu ujao.
0 Comments