LISSU AFUNGUKA KUHUSU CHADEMA KUINGILIA MGOGORO CUF, MADIWANI KUHAMIA CCM

LISSU AFUNGUKA KUHUSU CHADEMA KUINGILIA MGOGORO CUF, MADIWANI KUHAMIA CCM



Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu amefunguka kuhusu kitendo cha baadhi ya madiwani na wenyeviti wa chama hicho kuhamia CCM kutokana na hali ya kuridhishwa na uchapakazi wa Rais John Magufuli, na kudai kuwa viongozi hao wamekiuka sheria ya maadili ya viongozi wa umma ya mwaka 1997.

Wakati akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Lissu amedai kuwa, viongozi hao wamekiuka viapo vya maadili kwa sababu kuhama kwao kumesukumwa na rushwa.

Amedai kwamba, mmoja wa viongozi hao ambaye hakumtaja jina, wiki moja baada ya kuhamia CCM aliteuliwa kuwa Mchumi wa Halmashauri ya Arumeru, jambo ambalo amelifananisha na kula rushwa.

Katika hatua nyingine, Lissu amejibu tuhuma za baadhi ya wanasiasa, kuwa Chadema inaingilia mgogoro wa kiuongozi unaoendelea CUF. Amesema kwa kuwa chama hicho ni miongoni mwa vyama vinavyounda UKAWA, watahakikisha wanaingia vitani kumong’oa Prof. Ibrahim Lipumba aliyedai kuwa ni msaliti.

“Kuna CUF ya Maalim ambayo ilishinda viti vingi vya ubunge wakati wa uchaguzi, ambayo ni kitu kimoja na UKAWA, Kuna CUF ya Lipumba aliyenunuliwa ambaye hana tofauti na msaliti yuda eskarioti. CUF ya namna hiyo tuna vita nayo na tutaingia vitani kama tuliyo nayo kwa CCM,” amesema

Post a Comment

0 Comments