Ndoto za Rafael Nadal za yeyuka Wimbledon

Ndoto za Rafael Nadal za yeyuka Wimbledon


Ndoto za mcheza tenisi, Rafael Nadal kushinda mashindano ya Wimbledon kwa mara ya 3 mfululizo zimezimwa na Gilles Muller wa Luxembourg baada baada ya kukubali kichapo cha seti 6-3 6-4 3-6 4-6 na 15-13.


Mcheza tenisi,Rafael Nadal akionekana kuuzunika baada ya kutolewa mashindano ya Wimbledon

Bingwa huyo wa makombe makubwa mara 15 alionekana kuanza vyema mchezo huo kabla ya Muller kumgeuzia kibao na kushinda kwa jumla ya seti hizo ndani ya saa nne na dakika 47 pekee ya mchezo.


Muller mwenye umri wa miaka 34 anatarajia kucheza na Marin Cilic judoka nchini Crotia ambaye ni namba saba kwa viwango vya ubora wa mchezo huo duniani katika hatua ya nane bora.


Kwa kipigo hicho kunamfanya mchezaji huyo nyota wa mchezo wa tenisi kushindwa kuchukua kikombe hicho kwa mara tatu mfululizo kama alivyofanya kwa French Open.

Post a Comment

0 Comments