Rais Magufuli Atua uwanja wa mpira wa Lemela kumsubiri Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

Rais Magufuli Atua uwanja wa mpira wa Lemela kumsubiri Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza



Rais John Magufuli amewasili katika uwanja wa mpira wa Lemela Kata ya Kanazi Wilaya Ngara Mkoani Kagera ambapo atampokea Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza na baada ya hapo watakagua gwaride.


Mara baada ya kumaliza ukaguzi wa gwaride hilo viongozi hao watakuwa na maongezi maalum.


Rais Magufuli yuko ziarani Kanda ya ziwa na jana alizindua barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma- Biharamulo-Lusahunga.


Pamoja na uzinduzi Rais Magufuli pia alihutubia wananchi ambako umati mkubwa umehudhuria uzinduzi wa barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 154.

Post a Comment

0 Comments