Sasa hivi msanii huwezi kumdanganya shabiki – Climax Bibo

Sasa hivi msanii huwezi kumdanganya shabiki – Climax Bibo

Msanii wa Bongo Flava, Climax Bibo amedai kwa sasa ni vigumu kwa msanii kumdanganya shabiki na ndio sababu ya yeye kukaa kimya.


Climax ameeleza kutokana na mashabiki kufahamu vitu vingi msanii anapaswa kujipanga kikamilifu ili aweze kupokelewa vizuri ila atakapotaka kutoka kwa njia ya kiujanja hatofanikiwa.

“Game imebadilika na kuwa kubwa, kubwa sio kwamba kuna vitu vikubwa sana kwenye game, ni kwamba sasa hivi shabiki huwezi kumdanganya. Shabiki wa sasa hivi anafahamu mixing mbovu, anafahamu hii video haina quality, anafahamu hii video umecopy, anajua huyo msanii yupo kwa ajili ya kuji-brand, anajua msanii huyo ana uwezo mdogo, tofauti na game ya zamani,” ameiambia Daladala Beat ya Magic FM na kuongeza.

“Kwa hiyo mimi ni lazima nifanye kitu kikubwa mpaka mashibiki waseme, yes huyo ndiye Climax Bibo tunayemjua, kwa sababu hakuna asiyejua nina uwezo mkubwa. Unaona wasanii wakubwa wanatoa ngoma haziendi kwa sababu wanadanganya mashabiki pasipokujua wao wanaelewa,” amemaliza kwa kusema.

Post a Comment

0 Comments