Msanii Belle 9 amesema kuwa hana mpango wa kusaini msanii yoyote kwenye kampuni yake ya muziki ya Vitamini Music Group Limited.
Akiongea na mtangazaji wa kipindi cha Zero Planet cha Ice FM ya Njombe, Game Dee, muimbaji huyo amesema anamipango ya kufungua studio yake lakini hajafikiria kusaini wasanii wengine ndani ya kampui yake hiyo.
“Studio ni plan ambayo niliokuwa nayo lakini kusaini wasanii sijafikiria bado. Ninachofikiria ni kuwa support wasanii na sio mimi kama nawasimamia kila kitu, nataka nifanye kitu cha tofauti kidogo kwasababu wadau wa muziki wapo, kwa hiyo nitakua nasupport tu,” amesema Belle.
Kwa sasa muimbaji huyo amekuja na style mpya ya uachiaji wa ngoma mfululizo, tayari ameachia ngoma mpya iitwayo ‘Mfalme’ baada ya ‘Ma Ole’ aliouachia takribani miezi miwili iliyopita.
0 Comments