Vanessa Mdee kusuhu Jux, ‘alikuwa na vitabia vya ajabu ajabu’

Vanessa Mdee kusuhu Jux, ‘alikuwa na vitabia vya ajabu ajabu’



Baada ya kutemana na mpenzi wake msanii wa muziki wa Bongo Fleva, Vanessa Mdee amesema sababu kubwa ya kuachana mpenzi wake Jux ni kutokana na tabia zake ndogo ndogo ambazo aliona kwa baadae zingemuumiza zaidi.

Vanessa Mdee

Vanessa Mdee amesema alikuwa anamtumia meseji asubuhi na anaona ujumbe umefika ila haujibiwi anakuja kujibu mchana na jibu lenyewe ni kwa kifupi tuu so akaona ni heri akae chonjo.

“Unajua kuna tabia za kisela unakuta meseji inatumwa saa 12 asubuhi jibu unakuja kupata saa 6 mchana na zile tiki unaziona zinakuwa za blue inakuwaje sasa?… au mtu unamuuliza umekulaa yeye anajibu kwa kuguna, yanaweza kuwa sio mapenzi ya kisela ila vile vitabia tabia vinaashiria kuna kitu,“amesema Vanessa Mdee kwenye kipindi cha Chill na Sky.

Hata hivyo Vanessa Mdee amesema hana tatizo lolote na Jux na bado anampenda kama rafiki yake hawana tofauti zozote na anaamini hata Jux anampenda pia.

Post a Comment

0 Comments