Waziri, Mwakyembe amtumbua rasmi Malinzi

Waziri, Mwakyembe amtumbua rasmi Malinzi


Waziri wa Habari, Tamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe ametangaza kusitisha uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT).


Waziri wa Habari, Tamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe

Mwenyekiti wa Baraza hilo la Michezo Tanzania (BMT) , Dionis Malinzi, ambaye ni ndugu na Rais wa Shirikisho la Soka Jamali Malinzi uteuzi wake umesitishwa na Dkt Mwakyembe kufuatia agizo la Waziri Mkuu.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alimtaka Waziri Mwakyembe kupitia baraza hilo na kulitathimini hivyo baada ya kulipitia na kutathimini amesitisha uteuzi wa Mwenyekiti wa baraza hilo.


“Kwa mamlaka niliyopewa na sheria ya BMT Na.12 ya 1967, nimesitisha uteuzi wa Mwenyekiti na wajumbe wote wa BMT”-Dkt.Harrison Mwakyembe

Kwa mujibu wa Waziri Dkt. Mwakyembe amesema kuwa Sekretarieti ya Baraza la Michezo Tanzania litaendelea na kazi kwa kushirikiana na serikali wakati mchakato wa kuteua mwenyekiti mpya wa ukiendelea.


Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dionis Malinzi

Post a Comment

0 Comments