Wizara ya Afya yatangaza nafasi 3152 za ajira

Wizara ya Afya yatangaza nafasi 3152 za ajira


Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu 

Dar es Salaam. Wizara ya Afya, imetangaza nafasi za ajira 3152 kwa wahitimu katika kada mbalimbali za afya nchini.
Taarifa iliyotolewa jana na kuwekwa kwenye ukurasa wa Twitter wa Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu imeeleza kuwa, wizara ina jukumu la kuwapangia vituo waombaji wenye sifa kwa mujibu wa waraka wa maendeleo ya utumishi wa umma.
Miongoni mwa nafasi hizo, zipo za wauguzi daraja la kwanza na la pili, wapo wataalamu wa maabara, wanateknolojia na wataalamu wa lishe.

Post a Comment

0 Comments