SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER’S GORGE

SERIKALI KUTANGAZA ZABUNI YA MRADI WA STIEGLER’S GORGE


Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amesema kuanzia Agosti 30 mwaka huu, Serikali itatangaza zabuni ya kuanza ujenzi wa Mradi Mkubwa wa Umeme wa megawati 2100 katika maporomoko ya maji ya Mto Rufiji mkoani Pwani ( Stiegler’s Gorge)
Akizungumza jijini Dar es Salaam Dkt. Kalemani amesema, taratibu za awali zimeshaanza ambapo wataalaumu wa ndani na nje wameshakutana na kuchagua sehemu za kujenga mradi huo katika Mto Rufiji, ambapo tayari Shirika la Umeme Nchini ( Tanesco ) limeanza upembuzi yakinifu wa kujenga miundombinu ya umeme na Wakala wa barabara nchini (Tanroad) kujenga miundombinu ya barabara.
Ujenzi wa mradi wa umeme wa megawati 2100 kutoka maporoko ya maji ya Mto Rufiji Mkoani Pwani ( Stiegler’s Gorge)unatarajiwa kuanza ndani ya kipindi cha miezi miwili ijayo baada ya taratibu za zabuni kukamilika, Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dkt. Medard Kalemani amewambia watanzania kuwa, tayari Serikali imetenga fedha za kutekeleza mradi huo, na hatua za awali za utekelezaji zimekwisha fanyika, ambapo tarehe 30 ya mwezi huu wa Agosti Serikali itatangaza zabuni kwa wakandarasi wa ndani na nje ya nchi ili waweze kuomba kufanya kazi .
Dkt. Kalemani amesema mkandarasi atakayepewa kazi ya kujenga mradi huo ni yule tu atayeridhia kujenga kwa gharama nafuu na kwa muda mfupi zaidi ya uliowekwa.
Pia Dkt. Kalemani anatoa ufafanuzi namna ambavyo Serikali imejiandaa katika kutekeleza mradi huo.
mujibu wa Dkt Kalemani, mradi huo utakapokalimilika utakasaidia kuimarisha upatikanaji wa huduma ya umeme nchini na kwamba Serikali haitarajii kuongeza bei ya umeme.

Post a Comment

0 Comments