TPSF Yataja Sababu za Wafanyabiashara Kufunga Biashara Zao

TPSF Yataja Sababu za Wafanyabiashara Kufunga Biashara Zao


Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Sekta Binafsi Tanzania (TPSF), Godfrey Simbeye amesema kinachochangia kufa na kufungwa kwa biashara nchini kunatokana na mazingira magumu ya biashara pamoja na sera kandamizi zilizopo.

Amesema utafiti uliofanywa na TPSF umebaini kuwa biashara 4,640 zimefungwa nchini kwa kipindi cha miaka mitatu kutokana na vikwazo mbalimbali, huku akibainisha kuwa mfuko huo kwa sasa upo tayari kusaidia maeneo mbalimbali ya ujasiliamali pamoja na kutoa elimu.

Simbeye ametoa kauli hiyo jana Mei 17, 2018 katika kongamano la kambi ya ujasiriamali iliyoandaliwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe mkoani Morogoro.

Alisema Tanzania inatakiwa kupiga hatua zaidi katika suala ujasiriamali kwa sababu ni sekta pekee inayozalisha ajira kwa wingi nchini, hivyo ni vyema ikatumika kitaaluma katika kuwaandaa wanafunzi kufùndishwa kwa vitendo wanapokuwa vyuoni.

“Sekta binafsi ni mwajiri pekee wa kudumu katika maisha ya mtu ama watu hivyo vijana wetu wanatakiwa kuwa wathubutu na kuondokana na uwoga kwani ni tatizo kubwa kwa vijana wetu,”amlisema Simbeye.

Post a Comment

0 Comments