Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Atuma Salamu za Rambirambi Ajali ya MV Nyerere...Kasema Kenya Ipo Tayari Kutoa Msaada Wowote Utakaohitajika

Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta Atuma Salamu za Rambirambi Ajali ya MV Nyerere...Kasema Kenya Ipo Tayari Kutoa Msaada Wowote Utakaohitajika


RAIS wa Kenya Uhuru Kenyatta , ametuma salamu za rambirambi kufuatia vifo vya watu zaidi ya 100 waliofariki mpaka sasa kutokana na kivuko cha MV.Nyerere kupinduka Ziwa Victoria tarehe 20 Septemba 2018 

Katika ujumbe wake alioutuma katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter, Kenyatta ametoa pole kwa Watanzania kufuatia ajali hiyo.

“Kwa niaba yangu na wananchi wa Kenya, natuma salamu za rambirambi kwa ndugu yangu Rais Magufuli pamoja na majirani zetu raia wa Tanzania katika kipindi hiki kigumu kufuatia ajali ya kivuko cha MV Nyerere kilichozama Ziwa Victoria. ” amesema.
Rais Kenyatta amesema serikali yake ipo tayari kutoa msaada wowote utakaohitajika kufuatia ajali hiyo.



Kivuko hicho kilizama jana mchana Septemba 20, 2018 na hadi leo Septemba 21, 2018 maiti za watu 100 zimeopolewa.

Post a Comment

0 Comments