Uongozi wa Singida United wafanya mazungumzo na Manyika

Uongozi wa Singida United wafanya mazungumzo na Manyika



Uongozi wa klabu ya Singida United umesema upo kwenye mazungumzo na kipa wake, Peter Manyika ili aweze kurejea kikosini.

Manyika ameamua kujiengua ndani ya timu hiyo kutokana na kushindwa kulipwa stahiki zake ikiwemo fedha za usajili na mishahara ya miezi kadhaa.

Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa klabu hiyo, Festo Sanga, ameeleza kuwa bado wanahitaji zaidi huduma ya Manyika kwa sababu amekuwa msaada mzuri kwenye lango lao ili kukiimarisha kikosi.

Sanga anaamini Manyika watamrejesha kwa kufika naye pazuri kimazungumzo ambapo kwa sasa yupo jijini Dar es Salaam akijifua kwenye kituo cha baba yake mzazi ili kuendelea kulinda kiwango chake.

Kuondoka kwa Manyika ndani ya walima alizeti hao kumeanza kuipa taswira mbaya ambapo ukichana na kipa huyo inaelezwa kuna baadhi ya wachezaji wengine pia wanaidai klabu.

Post a Comment

0 Comments