Acha kiwe ‘Kitendawili’ ili kila mwenye jibu awe mshindi – Mrisho Mpoto

Acha kiwe ‘Kitendawili’ ili kila mwenye jibu awe mshindi – Mrisho Mpoto


Ni masaa 24 yamebaki ili msanii wa muziki wa asili nchini, Mrisho Mpoto aachie wimbo wake mpya ‘Kitendawili’ akiwa na mkali wa nyimbo za mahaba, Kassim Mganga ambapo mpaka sasa kwenye mitandao ya kijamii kumekuwa na maswali mengi huku wengi wakitaka kujua muimbaji huyo aachia wimbo wa namna gani.

Watangazaji wengi wa redio, runinga, wasomi, viongozi wa serikali pamoja wadau mbalimbali wamekuwa wakiweka vipande mbalimbali za video katika mitandao ya kijamii wakimzungumzia muimbaji huyo pamoja na ujio wake mpya hali ambayo imezua gumzo katika mitandao hiyo.

Akiongea na mwandishi wetu Jumatatu hii kuhusu fujo mbalimbali zinazoendelea katika mitandao ya kijamii, Mpoto amesema kabla ya wimbo huo haujatoka amekuwa akipokea maoni mbalimbali kutoka wa watu wake wa karibu pamoja na mashabiki wa muziki wake kupitia mitandao ya kijamii.

“Mungu amekuwa mkubwa sana, yaani wimbo bado haujatoka lakini tayari mashabiki wameanza kuhisi aina ya wimbo ambao unakuja. Watu wangu wa karibu pamoja na menejimenti yangu kila mmoja amekuwa na maoni yake kupitia mitandao ya kijamii na hii ni dalili nzuri katika muziki wangu na ujio mpya wa wimbo Kitendawili,” alisema Mpoto.

Aliongeza, “Acha kiwe Kitendawili mwenye jibu awe mshindi ndio maana nimekuwa nikisema huu wimbo tuache utoke kesho halafu tuangalie nini nimefanya, kwenye Sizonje watu walikuwa juu juu, hivyo hivyo lakini mwisho wa siku kila mtu akawa na jibu lake na mwisho wa siku wimbo ukafanya vizuri,”

Muimbaji huyo wakati atarajia kuaachia wimbo wake huo mpya hapo kesho, amesema baada ya siku chache video ya wimbo huo itaachiwa.

Wimbo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa muziki umeandaliwa na producer, Man Walter kutoka Combination Sound.

Post a Comment

0 Comments