Akamatwa kwa kumtishia Ariana Grande

Akamatwa kwa kumtishia Ariana Grande


Mwamaume mmoja mwenye miaka 22 amekamatwa kwa kumtishia maisha mwanamuziki Ariana Grande ambaye anatarajia kutumbuiza nchini Costa Rica.



Kwa mujibu wa habari zilizotolewa nchini humo na gazeti la La Nacion, zimeeleza kuwa mwanaume huyo amemtishia mwanamuziki Ariana mwenye miaka 24 kwa lugha ya kiarabu, ikiashiria kitendo cha hatari kutokea.

“A situation danger or an attack,” ameeleza msemaji wa kituo polisi Walter Espinoza. Pia vitisho hivyo vilitumwa kupitia njia ya simu kwenda kwa muimbaji huyo na simu aliyoitumia kufanya hivyo imekutwa nyumbani kwa mtuhumiwa.

Post a Comment

0 Comments