Aliyemwagwa na Simba SC ashinda tuzo ya mchezaji bora Rwanda

Aliyemwagwa na Simba SC ashinda tuzo ya mchezaji bora Rwanda



Kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba, Pierre Kwizera amebeba tuzo ya mwanasoka bora nchini Rwanda kwa msimu huu ikiwa na mara mbili mfululizo.

Pierre Kwizera akikabidhiwa tuzo ya mchezaji bora nchini Rwanda

Kwizera ambaye anakipiga kunako klabu ya Rayon Sports alitemwa na Simba SC kwa kile walichokidai kuwa mchezaji huyo ameshuka kiwango.

Mrundi huyo ambaye kwa msimu uliopita 2016/17 ametupia magoli 11 amekuwa moto wa kuotea mbali hii ni kutokana na mchango mkubwa wa utoaji pasi za mwisho zilizoipelekea klabu yake ya Rayon kuzima utawala wa klabu ya APR uliodumu kwa muda mrefu.

Post a Comment

0 Comments