Barcelona watwaa ubingwa wa kombe la kimataifa kwa kuichakaza Real Madrid (+Video)

Barcelona watwaa ubingwa wa kombe la kimataifa kwa kuichakaza Real Madrid (+Video)


Klabu ya Barcelona imeendeleza ubabe wa kombe la kimataifa kwa kuwafunga mahasimu wao Real Madrid magoli 3-2 na kutwaa ubingwa wa kombe hilo.


Goli la kwanza la Barcelona limefungwa na Lionel Messi dakika ya 3 na Ivan Rakitic dakika ya 6 kunako kipindi cha kwanza cha mchezo kabla ya Mateo Kovavic dakika 14 na Marco Ansesio dakika 36 kuisawazishia Real Madrid.

Goli la ushindi la Barcelona lilifungwa na beki wa kati wa klabu hiyo, Gerrad Pique kunako dakika ya 50 ya kipindi cha pili cha mchezo na ndiye aliyechaguliwa kuwa Man of the match huku mshambuliaji wa klabu hiyo, Neymar Jr akiibuka mfungaji wa michuano hiyo akiwa na magoli matatu.

Mchezo huo uliohudhuriwa na watazamaji 66,014 katika uwanja wa Hard Rock ulikuwa ni wa fainali ya Kombe la Mabingwa la kimataifa ambapo timu 8 kutoka mataifa mbalimbali zilishiriki na Barcelona wamefikisha pointi 9 kwa ushindi wa mechi zote tatu huku Real Madrid wakishika nafasi ya pili kwa pointi 6.

Hii inakuwa ni mara ya kwanza kwa Barcelona kutwaa kombe hilo linalofanyika kila mwaka nchini Marekani.

Post a Comment

0 Comments