Msanii mkongwe wa Bongo Flava, Dudu Baya amemjia juu msanii mwenzake Chege kwa madai anatumia jina lake la Konki.
Dudu Baya amedai kuwa Chege hana sifa za kutumia jina hilo kwani watu wanaotumia jina hilo ni wale wasiokata tamaa na kutokubali kushindwa.
“Sasa nimeshangaa nimesikia Chege naye anajiita Konki, Chege huna sifa za kujiita Konki. Konki ni watu ambao wanapambana, makonki ni watu ambao hawataki jamii ionewe, halafu nimesikia kuna mtu wa Bongo Movie nae anajiita Konki, naombeni majina yangu msiwe mnayaiga mimi ndiye Konki napambana mpaka tone la mwisho,” ameiambia Radio One na kuongeza.
“Unajua maana ya Konki, Konki ni mtu asiyekata tamaa, Konki ni mtu asiyekubali kushindwa, Konki ni mtu anayepigana hadi tone la mwisho kama Gaddafi na Libya,” amesema Dudu Baya.
Kipindi cha nyuma Dudu Baya aliingia katika mvutano na Shetta kwaa madai kuwa Shetta aliiga jina lake la Mamba.
By Peter Akaro
0 Comments