Davido aongoza chati za muziki Afrika

Davido aongoza chati za muziki Afrika

Msanii wa muziki Davido, ameongoza chati za MTV Base Afrika kupitia ngoma zake mbili.


Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram msanii huyo ameposti orodha ya nyimbo zote kumi zinazoongoza chati hiyo kwa siku ya jana huku yeye akishika namba moja kwa wimbo wa ‘Fall’ na namba tatu akiwa ni ya ‘If’ ambayo imefanyiwa remix na mkali R.Kelly.


“BLESSED! #ONEAFRICA @mtvbaseafrica BIG UP TO ALL AFRICAN ARTIST PUSHING THE CULTURE ! ALL BULLSHIT ASIDE ! WE CAN ALL WIN ! ,” ameandika Davido.

Kwa sasa msanii huyo anaendelea na ziara yake ya kimuziki ‘The 30 Billion World Tour’ inayojumuisha baadhi ya nchi za Bara la Afrika, Ulaya na Marekani.

Post a Comment

0 Comments