Eneka ni moja kati ya nyimbo ambazo Diamond ameziachia kwa kushtukiza na mapokezi yake yameonekana kuwa makubwa tofauti na alivyotarajia. Miongoni mwa walioonekana kuikubali ngoma hiyo ni Yemi Alade.
Kitendo cha Diamond kutumia baadhi ya maneno ya lugha ya nchini Nigeria ndio kimeonekana kumfanya Yemi kuupenda zaidi wimbo huo.
Muimbaji huyo kutoka huko Nigeria, ameshindwa kuzuia hisia zake kwa wimbo huo baada ya kucomment kwenye moja ya video ambayo Diamond ameiweka kwenye mtandao wa Instagram. “Omg !you are singing in IGBO @diamondplatnumz,” ameandika Yemi Alade.
Wimbo huo una siku mbili tangu umewekwa kwenye mtandao wa YouTube na tayari umeshatazamwa mara 252,616.
0 Comments