Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango. (kushoto), akikaribishwa na Afisa Udahili wa Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), Bw. Gerald Malisa, alipofika kutembeela banda la chuo hicho lililoko jengo la Wizara ya Fedha na Mipango, kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere, maarufu Sabasaba,barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam. Maonesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam yanaendelea kwenye viwanja hivyo na yatafikia kilele Julai 13, baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kuomba Tan Trade waongeze siku tano zaidi ili kutoa fursa pana kwa wanachi kutembelea maonesho hayo na kupata faida mbalimbali.
WAZIRI wa Fedha na Mipango, Dkt. Philip Mpango ametembeela banda la Chuo Cha Uhasibu Arusha, (IAA), lililoko kwenye jengo la Wizara ya Fedha na Mipango kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.
Waziri alikipongeza chuo hicho kwa maendeleo kilichofikia na kusaidia kutoa wataalamu katika Nyanja za uhasibu na utunzaji wa hesabu ambapo sasa kinaendelea kupanua huduma zake kwenye maeneo mengine nje ya makao makuu yake jijini Arusha.
Akimpatia maelzo waziri mpango, Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Sarah Goroi, alimueleza Waziri Mpango kuwa chuo hicho kwa sasa ukiacha makao makuu yake jijini Arusha pia kina matawi jijini Dar es Salaam, jijini Mwanza na wilayani Babati mkoa wa Manyara.
Sarah alisema, chuo kinatoa elimu ya uhasibu ngazi ya Astashahada(certificate), Stashahada(Diploma), Shahada ya Kwanza(Bachelor degree), Post Graduate diploma, na Shahada ya Uzamili (Masters Degree).




“Mheshimiwa waziri huduma tunazozitoa kwenye banda letu ni pamoja na kufanya udahili hapa hapa kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu mbalimbali zinazotolewa na chuo cheti kwa ngazi nilizozitaja.” Alifafanua Sarah




Alisema Mtu anayehitaji kujiunga na chuo hicho, afike kwenye banda la chuo akiwa na picha moja ya passport size ya rangi, na vivuli vya vyeti vya kidato cha nne, (Form Four), na Kidato cha Sita,(Form Six), kwa wale wanaoomba kujiunga na programu za Shahada ya Kwanza, au Cheti cha kuhitimu elimu ya Chuo Kikuu kwa wale wanaotaka kujiunga na programu za Masters.




Akieleza zaidi Sarah alisema, kwa wanafunzi wanaotaka kujiunga na programu za Astashahada (Cheti) wanapaswa wafike na vivuli vya vyeti vya kumaliza elimu ya sekondari (Kidato cha nne)




Chuo cha Uhasibu Arusha, ni taasisi ya kielimu iliyoanzishwa na sheria ya taasisi za elimu ya uhasibu Arusha ya mwaka 1990 (Act of 1990), udhibiti wa jumla na uongozi wa taasisi uko chini ya Baraza la Uongozi la chuo, (Governing Council), alifafanuaSarah..





Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC), anayeshughulikia masuala ya Siasa na Uhusinao wa Kimataifa, Kanali (mstaafu), Nelubinga, (kulia), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda hilo, huku Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Sarah Goroi(kushoto), akimsikiliza. Katikati ni Kanali Mstaafu, F.L Kakiziba.

Waziri Dkt. Mpango, akifurahia jambo wakati akipatiwa maeelzo kuhusu huduma za kielimu zitolewazo na Chuo hicho. Kulia ni Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho Sarah Goroi.



Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, (NEC), anayeshughulikia masuala ya Siasa na Uhusinao wa Kimataifa, Kanali (mstaafu), Nelubinga, (katikati), akizungumza jambo wakati alipotembelea banda hilo, huku Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo hicho, Sarah Goroi(kulia), akimsikiliza. Kushoto ni Kanali Mstaafu, F.L Kakiziba.





Dkt. Mpango, (kushoto), akisaini kitabu cha wageni kwenye banda hilo, wanaoshuhudia kutoka kulia ni Afisa Utawala wa chuo Bi. Sekunde Titus, Afisa Uadahili, Bw.Gerald Malisa, na Afisa Uhusiano na Masoko, Sarah Goroi.




Afisa Uhusiano na Masoko wa chuo cha Uhasibu Arusha Sarah Goroi akitoa maelezo kwa wateja waliofika katika banda lao kwenye viwanja vya Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam kunakofanyika maonesho ya 41 ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam.