Wanawake wengi hupata viuvimbe vilivyojaa maji kwenye tezi zao za kike (ovary cysts), mara nyingi viuvimbe hivi vinaweza kuwepo pasipo mwanamke kujua maana havileti maumivu wala athari kiafya. Baada ya muda, viuvimbe hivi hupotea vyenyewe bila tiba.



Hata hivyo, viuvimbe hivi haswa vile vinavyopasuka vinaweza kuleta athari mbaya kiafya. Ni muhimu kujua dalili hizi maana zinaweza kuleta matatizo makubwa ya kiafya.

Dalili moja wapo ni kujaa au kubanwa kwa tumbo na maumivu chini ya tumbo, upande ambapo kuna huo uvimbe mara kwa mara, maumivu ya nyonga, maumivu wakati wa kujamiiana, maumivu wakati wa haja kubwa, kutapika (au kuijisikia kutapika), kuendelea kujisikia tumbo limejaa, na kujisikia kwenda haja ndogo mara kwa mara.



Mwanamke akipata dalili hizo ni wakati wa kumwona daktari haraka iwezekanavyo, Inasemekana katika kesi nyingi za utasa, viuvimbe kwenye tezi za kike sio kisababishi , asilimia 40 ya kesi za utasa husababishwa na hitilafu katika shahawa za mwanaume.



Wakati pekee ambapo vivuvimbe hivi vinaweza pelekea utasa ni pale ambapo kuna maambukizi yanayoweza pelekea maambukizi kwenye pevic na kusababisha kuundwa kwa makovu kwenye tubes za fallopian. Kwa baadhi ya wanawake, makovu haya yanaweza kupelekea tatizo la utasa, ila kusema ukweli sio kitu common sana, hivyo hatuwezi kusema ovarian cyst husababisha tatizo la utasa.

Wanawake wenye vivimbe vilivyojaa maji kwenye tezi za kike (Ovarian cyst) huweza kupata madhara mabaya kutokana na uwepo wa vivimbe hivyo. Madhara hayo ni kama vile:

Vivimbe vinapopasuka huweza kusababisha damu kuvuja ndani ya mwili tatizo ambalo huwa vigumu kutambuliwa na hivyo kuhatarisha maisha ya mgonjwa. Kupasuka kwa vivimbe na kusababisha damu kuvuja ni tukio la dharura linalohitaji kutatuliwa haraka ili kuokoa maisha ya mgonjwa.

Kujikunja kunja kwa tezi za kike (Ovarian torsion) – hali ya kujikunja kwa tezi za kike hutokea kwa wagonjwa wengi wa Ovarian Cyst na ndio sababu kubwa ya wanawake kupoteza uwezo wa kubeba ujauzito. Kujikunja huko kunaweza sababisha mishipa ya damu nayo ikashindwa kufikisha damu kwenye sehemu zote za tezi ya kike na hivyo kusababisha eneo la tezi kufa hali inayoitwa Ovarian necrosis.

Kuvimba kwa kiwambo kinachofunika matumbo (Peritonitis) – Ikitokea vivimbe vikapasuka vinaweza sambaza viini vya maradhi kwenye eneo la matumbo ambavyo hushambulia kiwambo kinachozunguka matumbo na kusababisha kiwambo hicho kikavimba. Wagonywa wanaopata madhara haya hupata maumivu makali sana ya tumbo.

Ukosefu wa uwezo wa kubeba ujauzito/kuzaa (infertility) – ukosefu huu wa uwezo wa kubeba ujauzito huwa wa muda mfupi tu au wa kudumu kulingana na ukubwa madhara ya uwepo wa vivimbe vilivyojaa maji yaliyotokea kwenye mfumo mzima wa uzazi. Hii ina maanisha ni vyema kwa wanawake wote wenye dalili za uwepo wa vivimbe kufanya uchunguzi wa kina na kupata matibabu haraka ili kuepuka madhara mabaya yasiendelee kutokea na kuathiri mfumo wa uzazi.

Saratani – Ingawa hutokea mara chache sana lakini vivimbe hivi huweza kuwa saratani ya tezi za kike.
Msongo na sonona – maumivu makali ya tumbo pamoja na mabadiliko ya homoni yanayoambatana na vivimbe hivi huweza kusababisha mgonjwa kupata msongo wa mawazo ambao huweza kuishia kwenye maradhi ya sonona (depression).

Chanzo: Dr Isaac Maro