Kila kukicha ‘Grateful’ya Dj Khaled inazidi kuweka historia katika muziki, albamu hiyo ya kumi katika maisha ya muziki ya rapper huyo imeendela kukaa kileleni.
Kwa mujibu wa mtandao wa Billboard umepost na kuonesha albamu hiyo ikiongoza kwa wiki nyingine katika Chat za Billboard 200 albamu, huku nafasi ya pili ikishikwa na Calvin Harris kupitia alabamu yake ya ‘Funk Wav Bounces Vol.1′, huku nafasi ya tatu ikikamatwa na Kendrick Lamar kupitia albamu yake ya DAMN.
Grateful ni moja ya albamu iliyoshirikisha mastaa kibao akiwemo rapper Jay Z aliyetoa albamu yake ya 4:44 Juni 30 na kuweza kugika kiwango cha Platinum kwa siku chache, pia kuna wasanii kama Beyonce , Alicia Keys, Nas, Travis Scott, Rihanna, Niki Minaj, Chance The Rapper na wengine.
0 Comments