Ni siku nyingine tena tunakutana katika ulimwengu wa mitindo na kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani, na leo katika mitindo tutaangalia ni jinsi gani unavyoweza kutokelezea bila kuchukiza mtu katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu.
Katika kipindi hiki watu wengi wamekuwa wakijiuliza ni jinsi gani wanaweza kutokelezea ki-fashion, basi ondoa shaka kwani unaweza kutazama picha hapa chini na kujionea namna ambavyo unaweza kuvaa na ukapendeza katika kipindi hiki cha mwezi mtukufu wa Ramadhani.
Kwa upande wa mwanamke hakikisha basi unajisitiri vyema pia sio mbaya ukipaka make-up kwa mbali .
0 Comments