Haitham afafanua kwanini Wema Sepetu hakutokea kwenye video yake

Haitham afafanua kwanini Wema Sepetu hakutokea kwenye video yake

Msanii wa Bongo Fleva, Haitham amefafanua sababu ya Wema Sepetu kutoonekana katika video ya ngoma yake mpya ‘Play Boy’ ambayo amemshirikisha mrembo huyo.



Haitham amesema kulikuwa na mipango ya kufanya video na Wema na script ilikuwa tayari imeshaandikwa ila alipokosekana ilibidi wabadilishe.

“Na script ambayo tumefanya sasa inayoonekana kwenye video wasichana watatu ilibadilishwa fasta baada ya Wema kutokutokea kwenye video, so script ya mwanzo ambayo Wema alipaswa kuwepo aliandika yeye director na baada ya mabadiliko kutokea akabadilisha scrip,” ameiambia E-News ya EATV.

Kuhusu athari zilizojitokeza baada ya Wema kutokuwepo kwenye video, amesema “kwa upande wingine yameathiri kidogo sio sana kwa sababu kuna baadhi ya mashabiki wa Wema walitamani kumuona kwenye video, kwa hiyo ameathiri kidogo kwa wale mashabiki walikuwa wanatamani kumuona,” amesisitiza.

Play Boy ni ngoma ya pili kwa Wema Sepetu kushirikishwa na msanii wa Bongo Flava baada ya ile ya mwanzo ‘Shoga Yake Mama’ aliyopewa shavu na Snura, lakini hizo zote hakuna hata moja Wema ametokea kwenye video.

Post a Comment

0 Comments