Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema anapenda taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundation na si zinazohamasisha wanafunzi wazae kisha warudi shule.
Rais Magufuli ameyasema hayo Jumatatu hii, wakati wa uzinduzi wa nyumba 50 za wahudumu wa afya, zilizojengwa na Taasisi ya Mkapa Foundation.
“Nazipenda taasisi zinazohimiza maendeleo kama Mkapa Foundationa na si zinazotaka watu wazae halafu warudi shuleni. Mmekalia kusema kuwa watu wazae halafu warudi shule, sasa si watazaa kila mahali,” alihoji Rais Magufuli.
“Hata kwangu kuna watu wanaozaa na wala hawajabakwa, hata mtoto wa mdogo wangu alizaa bila kubakwa, alipoulizwa imekuwaje akajibu kwa kisukuma alafu akanizalia mtoto akamuita John, akakaa kidogo akazaa tena mtoto mwingine akamwita Samia,” alisema Rais Magufuli huku watu wakicheka.
0 Comments