Kiukweli mimi sifanyi kazi katika label yoyote – Young Killer

Kiukweli mimi sifanyi kazi katika label yoyote – Young Killer


Msanii wa hip hop Bongo, Young Killer ameendelea kusisitiza kuwa kwa sasa hayupo kwenye label yoyote.


Baada ya kutoa ngoma na Harmonize ‘Unaionaje’ kumekuwa na maswali mengi kutaka kujua iwapo msanii huyo amejiunga na label ya WCB licha ya hapo awali kutolea ufafanuzi suala hilo.

Kuendelea kusisitiza suala hilo Young Killer amesema, “kiukweli mimi sifanyi kazi katika label yoyote, nafanya kazi zangu mwenyewe lakini kuna watu ambao tunajaribu kushirikiana kufikisha muziki wetu pale ambapo tunahitaji kufika,” ameiambia Dj Show ya Radio One na kuongeza.

“Nimeshawahi kufuatwa na menejimenti tofauti tofauti na mameneja wa kujitengemea mmoja mmoja, hatukuweza kufika muhafaka au makubaliano ya kuhakikisha mimi naweza kuwa chini yao, so hatukuweza kufanikisha hilo zoezi, nafanya kazi mwenyewe ila kuna watu tunajaribu kusaidiana na wanajaribu kuniongoza,” amesema Young Killer.

Post a Comment

0 Comments