Elizabeth Michael ‘Lulu’ na mama yake Lucresia Karugila.
MAMA mzazi wa staa wa Bongo Muvi, Elizabeth Michael ‘Lulu’, Lucresia Karugila amezima minon’gono ya mwanaye huyo kutarajia kufunga ndoa akisema kuwa, mtoto wake huyo anajipanga kurudi darasani kwa ajili ya kujiendeleza kimasomo.
Akizungumza na Wikienda, mama Lulu alisema kuwa, kama mwanaye huyo angekuwa anaolewa kila mtu angejua kwa sababu ni jambo jema, lakini kwa sasa Lulu anajipanga kurudi Chuo cha Magogoni kilichopo Posta jijini Dar, kwa ajili ya kuendelea na masomo yake ya diplomasia.
“Lulu bado ni mdogo, ngoja asome kwanza maana ndoa ipo tu,” alisema mama Lulu.
0 Comments