Maua Sama adai mapenzi hayana vigezo

Maua Sama adai mapenzi hayana vigezo


Msanii wa Bongo Flava, Maua Sama amedai kuwa hakuna vigezo katika kuchagua mpenzi.


Hitmaker huyo wa ‘Main Chick’ ameiambia Daladala Beats ya Magic Fm kuwa mapenzi ni kuridhiana na kuendana hivyo unapotanguliza vigezo mbele si sawa kwani kila mtu ana udhaifu wake.

“Siku hizi hamna vigezo, mkiendana fresh; vigezo ni kama havina kazi cha msingi ni chemistry tunakuwa tunalindiana madhaifu, ukishasema vigezo vyangu how about me, mimi naweza nikawa na madhaifu yangu mengi tu anatakiwa kuyavumilia,” amesema Maua.

Katika hatua nyingine Maua ameeleza sababu kwa nini hamuweke wazi mpenzi wake ili mashabiki wake kumfahamu.

“Unajua ukiweka mahusiano wazi yanakuwa ya watu hayawi yako tena mwenyewe kwa hiyo mwisho wa siku inakuwa mnapangiwa watoto, what should be to do, hivyo watu wanakuwa wanawapangia, wanataka kujua mkiachana itakuwaje,” amesisitiza.

Post a Comment

0 Comments