USAJILI: Yanga SC yamalizana na Kamusoko

USAJILI: Yanga SC yamalizana na Kamusoko


Mabingwa mara tatu mfululizo wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara klabu ya Yanga imemsainisha Mzimbabwe, Thaban Scara Kamusoko kwa mkataba wa miaka miwili kuendelea kuwatumikia mabingwa hao wa kihistoria.


Klabu ya Yanga imemsainisha mkataba wa miaka miwili Mzimbabwe, Thaban Scara Kamusoko 

Kamusoko ndiye mchezaji pekee ambaye hakuwa na uhakika wa kuendelea kuichezea Yanga msimu ujao kati ya waliokuwepo kwenye kikosi cha timu hiyo msimu uliopita, ambao wapo kwenye mipango ya kocha Mzambia George Lwandamina.

Mpaka sasa jumla ya wachezaji 16 ndiyo wapo mazoezini wakiwa katika maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano mingine.

Miongoni mwa hao ni pamoja na wachezaji wapya wanne, kipa Mcameroon, Youthe Rostand aliyesajiliwa kutoka African Lyon, beki Abdallah Hajji ‘Ninja’ kutoka Taifa Jang’ombe, kiungo Pius Buswita kutoka Mbao FC na mshambuliaji Ibrahim Ajib kutoka kwa mahasimu, Simba SC.

Wengine ni mabeki, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Juma Abdul, Pato Ngonyani, Mwinyi Hajji Mngwali, Andrew Vincent ‘Dante’, viungo Geoffrey Mwashiuya, Juma Mahadhi, Said Juma Makapu, Emmanuel Martin, Yussuf Mhilu, Obrey Chirwa na mshambuliaji Amissi Tambwe.

Post a Comment

0 Comments