Mchezaji wa zamani wa klabu ya Manchester United, Philip Mulryne ameamua kuachana na soka na kujaribu maisha ya mengine ya kitume kwa kugeukia Upadri.
Askofu Joseph Augustine Di Noia akimpadrisha Philip Mulryne
Philip Mulryne (39) amepata upadrisho mbele ya Askofu Joseph Augustine Di Noia jumamosi ya wikiendi iliyopita katika jimbo katoliki la Dublin nchini Ireland .
Katika maisha yake ya soka Philip Murlryne ameitumikia timu yake ya Taifa ya Ireland ya Kaskazini kwa kushinda michezo 27 ukiachana na mechi alizoshinda kwenye vilabu vya Norwich City na Leyton Orient.
Padri Mulryne maisha yake ndani ya klabu ya Manchester United safari yake ilianza mwaka 1994 alipojiunga na timu ya vijana na mwaka mmoja baadae 1995 alitwaa kombe la FA la vijana (FA Youth Cup) na kuanza kuamini katika soka.
Mwaka 1997, Philip Murlyne aliaminiwa na kocha wa Manchester United wa kipindi hicho, Sir Alex Ferguson kwa kuanza kwenye timu ya wakubwa kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Ipswich City mechi ambayo iliisha kwa Man United kupigwa goli 2-0.
Tangia hapo changamoto za kupata nafasi kwenye kikosi cha timu ya wakubwa hususani katika safu ya ushambuliaji ikaanza kuwa ngumu hii ni kutokana na ushindani wa nafasi hiyo ambapo alikuwa anashindana na wakali wengine kama David Beckham, Nicky Butt, Paul Scholes, Andy Cole na Ole Gunnar Solskjaer.
Padri Mulryne ndani ya msimu huo (1997-98) alicheza mechi moja tu ya Ligi kuu England dhidi ya Barnsley kabla ya kutemana na Man united na kuelekea Norwich City kwa dau £500,000 mwaka 1999 .
Murlyne alitangaza kutundika Daruga mwaka 2009 na baadaye kuanza masomo yake ya Upadri katika chuo cha Mtakatifu Malachy’s Belfast huko Ireland ya Kaskazini na baadae kuhitimu masomo yake ya Saikolojia na Theolojia katika vyuo vya Queens University Belfast na Pontifical Irish College cha jijini Roma, Italia .

0 Comments