Wachezaji tenisi raia wa Uingereza, Andy Murray na Johanna Konta wanatarajia kuingia uwanjani leo kuiwakilisha Uingereza katika michuano ya Wimbledon ya wanaume na wanawake.


Konta (kulia) hajawahi kushinda taji la Wimbledon

Wachezaji has wataingia uwanjani huku wakihakikisha wanashinda na kuingia hatua ya Robo fainali ya michuano hiyo mikubwa na kama watafanikiwa itakuwa ndio kwa mara ya kwanza Uingereza kufanya hivyo tokea mwaka 1973.

Konta atapambana na Caroline Garcia katika mchezo wa ufunguzi. wakati bingwa mtetezi Murray yeye atacheza na Benoit Paire.

Wachezaji Roger Federer, Novak Djokovic, Rafael Nadal na Murray kwa pamoja wameshinda vikombe 14 vya Wimbledon, huku mshindi mara tano Venus Williams akiwa ndiye pekee aliyeng’ara kwa upande wa kinadada.