Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafanya upasuaji zaidi wagonjwa 600

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete yafanya upasuaji zaidi wagonjwa 600


Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI ni hospitali ya pili kwa kupasua wagonjwa wengi wa moyo barani Afrika huku ikiongoza pia kwa upasuaji salama, ambapo kwa mwaka huu 2018, jumla ya wagonjwa elfu moja wanatarajiwa kufanyiwa upasuaji, kati ya hao 620 tayari wameshafanyiwa upasuaji.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo,. Prof Mohammed Janabi amebainisha hayo jijini Dar es salaam muda mfupi baada ya umoja wa wake wa viongozi nchini wakiongozwa na mke wa waziri mkuu Mary Majaliwa kutoa msaada wa hundi ya Shs Millionu nne ili kusaidia watoto wawili kufanyiwa upasuaji wa moyo kwenye taasisi hiyo.

Prof Janabi amebainisha zaidi kwamba mwaka jana pekee taasisi yake hiyo ilifanya upasuaji kwa wagonjwa mia tatu na hamsini na hivyo kushika namba mbili barani afrika, huku kati ya wagonjwa mia moja wanaopasuliwa vifo ni asilimia nane nukta sita, wakati wastani wa kawaida ni vifo asilimia 13, na taasisi nyingine barani afrika zimefikisha vifo asilimia 23, hivyo taasisi ya Jakaya Kikwete ni miongoni mwa hospitali za moyo ambazo zinaongoza kwa upasuaji salama.

Naye mke wa waziri mkuu mama Mary Majaliwa ameishukuru serikali kwa jitihada zake katika sekta ya afya hasa uboreshaji wa huduma za afya ya mama na mtoto.

Post a Comment

0 Comments