Nilifanya mazoezi ya riadha wiki moja kwa ajili ya Rooney – Shabiki aliyemkumbatia Wayne Rooney (+video)

Nilifanya mazoezi ya riadha wiki moja kwa ajili ya Rooney – Shabiki aliyemkumbatia Wayne Rooney (+video)


Shabiki aliyemkumbatia mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Manchester united, Wayne Rooney amesema mpaka kutekeleza tukio hilo alifanya mazoezi ya riadha kwa wiki moja asubuhi na mchana.

Shabiki Hassani Omar akimvamia Rooney.

Shabiki huyo wa kutupwa wa Manchester United aliyejitambulisha kwa jina la Hassan Omar amesema alivyosikia Rooney anakuja nchini aliwambia marafiki zake kuwa ni lazima akutane na Rooney ingawaje marafiki zake walimbeza.

“Ilikuwa ni lazima iwe vile kutokana kwanza nina mapenzi ya dhati na mchezaji yule japokuwa ameondoka kwenye timu yetu lakini kwa épande wangu mapenzi yang yapo pale pale…Niliposikia Rooney anakuja na timu yake mpya nikawambia marafiki zangu kuwa ni lazima nitafanya tukio la kumkumbatia Rooney”,amesema Hassan Omar huku akiendelea kuelezea jinsi alivyojiandaa na tukio hilo.

“Nilifanya mazoezi ya kukimbia asubuhi na jioni kwa muda wa siku tano baada ya hapo nilijiandaa vizuri na lengo likiwa sikutaka kukamatwa kabla ya kumkumbatia Rooney “,amesema Omar kwenye mahojiano yake na Gazeti la Mtanzania.

Hata Hivyo shabiki huyo amesema hakupigwa hata kofi na askari ingawaje watu wengi wanafikiri kuwa alipigwa na maaskari baada ya tukio hilo la kumkumbatia Rooney.

“Hayo manna ya kupigwa sio ya kweli sijapigwa mimi sikuguswa hata kidogo yaani kwanza siamini kama nilienda sero kwa sabbat naingia mle ndani watu wananishangilia kama wananijua“,amesema omar.

Wayne Rooney alikuja nchini Tanzania Tar 13 Julai mwaka huu na timu yake mpya ya Everton kisha kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Klabu ya Gor Mahia kutoka Kenya mchezo ambao uliisha kwa Everton kuibuka kwa ushindi wa goli 2-1 .

Tazama mahojiano yake yote hapa chini na Gazeti la Mtanzania .

Post a Comment

0 Comments