USAJILI: Simba SC yango’a kiungo hatari wa Azam dakika za majeruhi

USAJILI: Simba SC yango’a kiungo hatari wa Azam dakika za majeruhi


Bingwa wa kombe la FA klabu ya Simba imethibitisha kumsajili kiungo kiraka ambaye anaweza kucheza nafasi zote za ulinzi, Erasto Nyoni kutoka Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili baada ya mchezaji huyo kumaliza mkataba wake.


Simba ambayo inajiimarisha kwaajili ya msimu ujao wa ligi na mashindano ya kimataifa mpaka sasa imefanikiwa kuwasajili wachezaji golikipa Aishi Manula , beki Shomari Kapombe, mshambuliaji John Bocco wote kutokea Azam FC, Emmanuel Okwi akitokea Uganda, Ammanuel Mseja, Ally Shomari, Saidi Mohamed huku wakitarajiwa kumuingiza kikosini mchezaji Haruna Niyonzima.

Post a Comment

0 Comments