Quick Rocka akana kupanga ‘kiki’ na TID

Quick Rocka akana kupanga ‘kiki’ na TID

Msanii wa Bongo Flava, Quick Racka amesema si kweli kwamba kitendo cha TID kumtuhumu hadharani yeye na OMG kuchukua ngoma ya ‘Watasema Sana’ ni kitu walikua wamepanga pamoja ili kuipa kiki ngoma waliyotoa ‘Watasema’.


Quick Rocka amefunguka hayo kupitia kipindi cha Ladha 3600 cha E Fm kwa kueleza kuwa mawasiliano na TID yalikuwa yameshafanyika ila kuna mambo mwishoni yalikuja kuingiliana.

“Hapana haikuwa mipango, ilitokea na kwa jinsi ilivyotokea ilikuwa ni ghafla sana coz wakati tunafanya huu wimbo kuna siku nilimpa taarifa Mnyama kwamba kuna ngoma yako fulani ya zamani tunataka tuirudie, akasema fresh itakavyokuwa mtaniambia,” amesema Quick na kuongeza.

“Lakini baada ya hapo tumeshaifanya tumeanza kushoot video yeye alikuwa hayupo alikuwa Zambia or Burundi, kwa hiyo hadi tunaitoa yeye alikuwa hayupo, amerudi kama siku moja hivi sisi tumeitoa,” ameeleza Quick.

Kipindi cha nyuma TID alimjia juu Quick Rocka na kundi la OMG kwa madai ya kutumia ngoma yake ‘Watasema Sana’ bila ruhusa kutoka kwake, hata hivyo jambo hilo walikuja kulimaliza kwa pamoja.

Post a Comment

0 Comments