USAJILI: Tetesi za usajili barani ulaya

USAJILI: Tetesi za usajili barani ulaya

Everton wametoa dau jipya la pauni milioni 32 kumpata kiungo wa Swansea, Gylfi Sigurdsson mwenye umri wa miaka 27. Wakifanikiwa watakuwa wametuia zaidi ya pauni milioni 100 za usajili msimu huu (Daily Mail).


Mchezaji wa Swansea, Gylfi Sigurdsson

Baada ya kumsajili Romelu Lukaku, 24, kutoka Everton, Manchester United huenda wakamsajili kiungo wa Monaco, Tiemoue Bakayoko mwenye umri wa miaka 22, baada ya kukubaliana mkataba wa pauni milioni 35, Chelsea nayo inataka huduma ya mchezaji huyo (Daily Star).


Mchezaji wa Monaco, Tiemoue Bakayoko

Arsenal wapo tayari kupanda dau la zaidi ya pauni milioni 45 kumpata winga wa Monaco, Thomas Lemar baada ya dau la pauni milioni 30 na 40 kukataliwa (Daily Mirror).

Mshambuliaji wa Arsenal, Theo Walcott mwenye umri wa miaka 28, amedhamiria kupigania nafasi yake Emirates, licha ya kuhusishwa na kuhamia West Ham kwa pauni milioni 20 (Daily Star).

Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger anataka kuimarisha eneo la kiungo kwa kumsajili Marcelo Brozovic kutoka Inter Milan (ESPN).


Mchezaji wa Inter Milan, Marcelo Brozovic 

Kipa wa Arsenal, Wojciech Szczesny mwenye umri wa miaka 27, ambaye amehusishwa na kuhamia Juventus, ameachwa kwenye kikosi kilichosafiri kwenda Australia kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya (Sun).

Chelsea wapo tayari kutoa euro milioni 80 kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid, Alvaro Morata baada ya kumkosa Romelu Lukaku (AS).

Meneja wa Tottenham, Mauricio Pochettino anataka kumsajili beki wa Estudiantes, Juan Foyth mwenye umri wa miaka 19 kwa pauni milioni 10 (Daily Mirror).

Real Madrid wapo tayari kumuuza kiungo, Mateo Kovacic, na Tottenham wamehusishwa na kumchukua mchezaji huyo wa kimataifa wa Croatia (Evening Standard).


Mchezaji wa Real Madrid, Mateo Kovacic

Newcastle wanajaribu kukamilisha usajili wa kiungo wa Norwich Jacob Murphy, 22, kwa pauni milioni 8.5, huku Southampton na Crystal Palace wakimtaka pia mchezaji huyo (Daily Mirror).

Post a Comment

0 Comments