Wayne Rooney aanza mazoezi rasmi Everton

Wayne Rooney aanza mazoezi rasmi Everton


Nyota wa klabu ya Everton FC, Wayne Rooney ameanza mazoezi na timu yake huku akiwa na shauku kubwa ya kutua Tanzania kwaajili ya mchezo wake wa kirafiki dhidi ya Gor Mahia utakaopigwa katika nimba la Taifa jijini Dar es salaam Julai 13 mwaka huu chini ya udhamini wa Kampuni ya kubashiri michezo ya SportPesa.


Timu ya Everton ikiwa katina mazoezi na baadhi ya nyota wake wapya akiwemo, Wayne Rooney

Everton inatarajia kutua Tanzania kukipiga dhidi ya Wakenya hao katika kukamilisha michuano ya SportPesa Super Cup ambayo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar iliyoshirikisha timu kadhaa.

Rooney ambaye ndie mfungaji wa muda wote ndani ya klabu ya United baada ya kuichezea michezo 559 na kufunga mabao 253 na kurudi Everton tangu anodeke miaka 13 iliyopita amesisitiza kuwa miongoni mwa wachezaji watakao kuja nchini, kuanza mazoezi ya pamoja na wenzake, amesema kuwa atakuwemo kwenye msafara huo chini ya Kocha Ronald Koeman.



Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 alijiunga na Toffee alipokuwa na umri wa miaka 9 pekee ndani ya viunga hivyo vya Goodison kisha kujiunga na United mwaka 2004 na kuwasaidia kutwaa mataji ya Champions League, Europa League, mataji Nagano ya Premier League , mojo la FA Cup, matatu ya League Cups na moja la FIFA Club World Cup.




Muonekano mpya wa Rooney

Na kwa rasa mchezaji huyo anaeongoza kwa idadi ya magoli katika timu ya taifa ya Uingereza amefungua ukurasa mpya The Blues.

Post a Comment

0 Comments