Video: Mayweather amchapa mpinzani wake kwa noti kabla ya pambano lao

Video: Mayweather amchapa mpinzani wake kwa noti kabla ya pambano lao


Homa ya pambano la masumbwi baina ya mfalme wa uzito wa welter, Floyd Mayweather dhidi ya Conor McGregor inazidi kupamba moto mara baada ya bondia huyo wa Marekani usiku wa jana kumwagia noti za dola za Kimarekani mpinzani wake mara baada ya kukutana katika mkutano wao na waandishi wa habari.


Floyd Mayweather (mbele kushoto) akimwagia dola za kimarekani, Conor McGregor (aliyekaa kulia)

Mayweather ambaye alistaafu masumbwi mwaka 2015 akiwa na rekodi ya kutopoteza pambano hata moja kati ya michezo 49 aliyowahi kucheza anatarajia kukutana na McGregor ulingoni huko Las Vegas Agosti 26, mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments