Waziri Nchemba aagizwa kusitisha kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi

Waziri Nchemba aagizwa kusitisha kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amemuagiza Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba kusimamisha kutowapa uraia raia wa Burundi kuanzia sasa.


Rais Magufuli ameyazungumza hayo leo, wakati wa ziara yake mkoani Kagera, akiwa na mgeni wake Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza

“Kwa hiyo na mimi nawaomba wakimbizi kwa hiari yao warudi Burundi mimi siwafukuzi ila kwa hiari yao warudi nyumbani. Nimesikia wakimbizi wengine wameahidiwa kupewa elfu kumi kumi wabaki sasa nasema wakawapeni hizo hela mkiwa Burundi,” amesema Rais Magufuli.

“Rais amezungumza hapa kwa upole, Rais mwenyewe ana hofu ya Mungu, wazazi wake waliuawa, lakini anataka kushirikiana na Warundi wote kwa nini mnataka kuondoka kwenu,” amesema.

Post a Comment

0 Comments