Sababu za kiufundi zamkwamisha Abdu Kiba kutoa ngoma

Sababu za kiufundi zamkwamisha Abdu Kiba kutoa ngoma


Msanii wa Bongo Flava, Abdu Kiba ametaja sababu ya kukaa kimya kwa muda mrefu bila kutoa ngoma.


Muimbaji huyo ambaye mara ya mwisho alidondosha hit song akiwa na Ruby ‘Ayayaa’, ameiambia XXL ya Clouds Fm kuwa tatizo la kiufundi limepelekea kukaa kimya bila kutoa ngoma.

“Ni kutokana na sababu za kiufundi ambazo zipo chini ya menejimenti ya Kings Music, nikutokana na mpangilio wa kazi na program jinsi zilivyotubana lakini kila kitu kipo sawa na ngoma zipo nyingi za kutosha, so zitakapokuwa tayari watapokea ngoma za kutosha kutoka Kings Music, kutoka Kiba Squared,” amesema Abdu Kiba.

Post a Comment

0 Comments