Bolt afananishwa na bondia Muhammed Ali

Bolt afananishwa na bondia Muhammed Ali


Rais wa Shirikisho la riadha duniani (IAAF), Sebastian Coe amesema kuwa, Usain Bolt ana kipaji na ana ushawishi mkubwa miongoni mwa wanariadha kama, Muhammed Ali alivyokuwa na ushawishi miongoni mwa mabondia


Mwanariadha raia wa Jamaica, Usain Bolt

Mwanariadha huyo raia wa Jamaica Bolt ni bingwa wa mbio fupi ambaye ameshinda medali ya dhabau katika michezo ya olimpiki mara nane anatarajiwa kustaafu baada ya mashindano ya ubingwa mjini London yalioanza siku ya Ijumaa.

Coe alimfananisha Bolt na bondia mashauri duniani, Muhammed Ali.

Bingwa wa uzito wa juu, Muhammad Ali akiwa amesimama na mpinzani wake, Sonny Liston akiawachina akishindwa hata kuamka katika pambano lililofanyika May 25, 1965, huko Lewiston, Maine.

“Usain Bolt ana kipaji.siwezi kumfananisha na mwanamichezo mwengine yeyote yule zaidi ya Muhammad Ali, ambaye amekuwa na ushaiwishi mkubwa nje na ndani ya michezo”, amesema Coe ambaye ni rais wa IAAF.

Sebastian Coe ameongeza kwa kusema kuwa “Unaweza kuanzisha mjadala kuhusu ni nani mchezaji bora wa soka duniani ama mchezaji wa tenisi bora, lakini hakuna mjadala kuhusu Bolt katika mbio fupi”.




Bingwa wa uzito wa juu, Muhammad Ali akimfokea mpinzani wake asimame aendelee na mpambano

Usain Bolt ni bingwa wa mbio za mita100, 200 katika michezo ya Olimpiki iliyofanyika mjini Beijing mwaka 2008 na mjini London Uingereza mwaka 2012 na mjini Rio nchini Brazili mwaka 2016.


Mwanariadha raia wa Jamaica, Usain Bolt

Post a Comment

0 Comments