Dayna Nyange achukulia poa tambo za Shilole

Dayna Nyange achukulia poa tambo za Shilole


Msanii wa Bongo Flava, Dayna Nyange amesema hakuna msanii ambaye anaweza kufanya kitu na kuweza kuwapoteza wasanii wengine.


Kauli hiyo ni jibu kwa Shilole ambaye wakati anakaribia kutoa wimbo ‘Kigori’ alidai amewapa nafasi wasanii wa kike lakini wameshindwa kufanya vizuri hivyo anakuja kulichukua game

“Mimi nafikiri yeye ndio anaweza kuwa majibu yote kwamba kwa nini amekuja kuchukua game yake, labda alikuwa kimya kwa muda mrefu akawa anaona bado nafasi yake ipo. Unajua kila mmoja ana riziki yake kwenye hizi kazi usitengemee kwamba Dayna atakuja kufanya kitu fulani nimpoteze mtu fulani, hapana kila mta na riziki yake na kila mja na wakati wake,” ameiambia E-Newz ya EATV na kuongeza.

“I think ni wakati wake kama alifanya kitu fulani akaona mafanikio yake lakini akaona huku bado kulikuwa na mafanikio yake au anahitaji zaidi, so ana haki ya kufanya, kusema anachuku game ni misamiti tu ya lugha zetu za kisanii,” amesema Dayna.

Kuhusu lini atatoa ngoma mpya amesema, “watu wameona kimya baada ya kuachia Komela, lakini niseme always sipendi kukurupuka napenda nifanye kila kitu kwa wakati kiwe kizuri zaidi ya Komela, so very soon Mungu akijalia kazi yangu mpya itakuja,” amesema Dayna.

Post a Comment

0 Comments