Ikiwa zimepita siku kadhaa toka msanii kutoka Nigeria, Patoranking kuonyesha picha akiwa na mtoto katika mtandao wa Instagram na kuanza kuzua utata, sasa siri ya picha hiyo yafahamika.
Imefahamika kuwa msanii huyo alikuwa anapigia promo ngoma yake mpya iitwayo ‘Love You Die’ aliomshirikisha Diamond Platnumz ambao unatarajiwa kutoka Septemba 1 ya mwaka huu.
Patoranking na Diamond Platnumz katika utengenezaji wa video mpya
Kwa sasa Patoranking anahit na ngoma yake ‘This Kind Love’ aliyomshirikisha Wizkid ambayo imetoka mwezi huu kwenye mtandao wa YouTube na mpaka sasa imefikisha views 1,918,056.
0 Comments