Na.Ahmad Mmow,Nachingwea
HALMASHAURI ya wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi,imetenga jumla ya shilingi 219 .00 milioni zinazotokana na na mapato yake ndani kwa ajili ya ukarabati wa soko la wilaya, soko dogo la voda na ujenzi wa ya maegesho ya magarivkatika kituo kipya cha mabasi.
Hayo yalielezwa hivi karibuni na mwenyekiti wa halmashauri hiyo,Ahmad Makoroganya,wakati anazungumz a na wananchi wa kata ya Nachingwea kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika viwanja vya maulidi mjini Nachingwea.
Makoroganya alisema kwakutambua umuhimu wa soko kuu hilo kwa wakazi wananchi wa wilaya ya Nachingwea na nje ya wilaya hiyo .Halmashauri hiyo imetenga shilingi 135.00 milioni kwa ajili ya kulifanyia ukarabati.Huku shilingi 18.00 milioni zikitengwa kwa ajili ya ukarabati wa soko dogo la Voda.
"Tulichelewa kuanza ukarabati wa soku kuu ili tuanze kukarabati soko la Voda ili huduma zisisimame wakati tunalifanyia ukarabati.Wakati tunafanya ukarabati watoa huduma itabidi wahamie soko la Voda,"alisema Makoroganya.
Licha ya ukarabati wa masoko hayo ,mwenyekiti huyo ambae pia ni diwani wa kata ya Ugawaji anaetokana na Chama Cha Mapinduzi(CCM) alisema ujenzi wa kituo kipya cha mabasi upo katika hatua za mwisho kukamilika.Ambapo hivi sasa bado kukamilisha ujenzi wa maegesho tu.Huku akibainisha kuwa Nazi hiyo imetengewa shilingi 66.00 milioni.
"Sio hayo tu, halmashauri imeendelea kupeleka fedha kwenye vikundi vya ujasiriamali vya wanawake na vijana.Hadi sasa vikundi 34 vya wanawake na 24 vya vijana vimepewa mikopo.Changamoto ni urejeshaji wa mikopo hiyo ,kuna watu wanachukulia mikopo hiyo kama hisani,"alifafanunua na kulalamika Makoroganya.
Katika hali inayoonesha halmashauri hiyo imejizatiti kupeleka fedha hizo zinazotokana na mapato yake ya ndani, mwekiti huyo aliongeza kusema imeamua kuingiza fedha kwenye akaunti ya mfuko wa vijana na wanawake kila mwezi badala ya kila robo mwaka ya mwaka wa fedha.
Halmashauri ya wilaya ya Nachingwea ni miongoni mwa halmashauri zilizovuka lengo la ukusanyaji wa mapato kupitia vyanzo vyake vya ndani.Ambapo katika mwaka wa fedha wa 2016/2017 ilivuka lengo kwa kufikia asilimia 105.
Halmashauri nyingine zilizopo katika mkoa wa Lindi ni Liwale,Kilwa,Ruangwa,Lindi vijijini na Manispaa ya Lindi.
0 Comments