Arusha. Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira amewaongoza wakazi wa mkoa huo kuwapokea wanafunzi watatu wa shule ya Lucky Vincent waliowasili asubuhi hii kutoka Marekani.
Wanafunzi waliorejea ni Doreen mshana,Sadia Awadh na Wilson Tarimo
Wanafunzi hao walianza kushuka mmoja mmoja kutoka kwenye ndege hiyo.
Wanafunzi hao manusura wa ajali iliyotokea mwezi wa tano wamelakiwa na umati wa watu wakiwamo Wanafunzi wenzao wa shule ya Lucky Vicent.
0 Comments