Taarifa ya serikali kuhusu madai ya raia 16 wa Somalia, Pakistan na Lebanon kukamatwa uwanja wa ndege Dar.

Taarifa ya serikali kuhusu madai ya raia 16 wa Somalia, Pakistan na Lebanon kukamatwa uwanja wa ndege Dar.



Tarehe 31/07/2017 chombo kimoja cha habari kilitoa taarifa za upotoshaji kwamba wageni 16 wenye uraia wa Lebanon, Pakistani na Somalia walinaswa katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) baada ya kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP).


Taarifa sahihi za suala hili ni kwamba Tarehe 30107/2017 abiria wanne (4) Raia wa Taifa la Pakistan waliwasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa eha Julius Nyerere (JNlA) na kupita Jengo la Watu Mashuhuri (VIP Lounge) ambapo nyaraka zao za safari zilikaguliwa na Maafisa wa Uhamiaji na baadae kuruhusiwa kuingia nchini baada ya kujiridhisha kuwa ni halali. 


Abiria hao walikuwa na kibali kinachowaruhusu kutumia ukumbi wa watu mashuhuri (VIP) kilichotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.


Utaratibu uliopo katika matumizi ya Ukumbi wa watu Mashuhuri (VIP Lounge) JNIA ni kwamba wageni wote toka nje ya nehi wanaohitaji kutumia ukumbi huo wanalazirnika kuomba kibali Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa na Wizara husika inapojiridhisha na vigezo vya waombaji,hutoa vibali hivyo.


Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) inatoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuandika habari kwa weledi na kuhusisha pande zote zinazohusishwa katika taarifa zao mbalimbali, ili kuepuka mkanganyiko na upotoshaji kwa jamii kwa jambo husika.


TAA ipo tayari kutoa ushirikiano kwa chombo chochote cha habari kinachowasiliana nacho kutaka ufafanuzi wajambo fulani, iii waweze kuandika kwa umakini na ufasaha zaidi.


IMETOLEW ANA:


KAIMU MKURUGENZI MKUU WA MAMLAKA YA VIWANJA VY A NDEGE TANZANIA (TAA)

Post a Comment

0 Comments