Wachimbaji waishitaki Tanzanite One bungeni

Wachimbaji waishitaki Tanzanite One bungeni



Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani 

WAFANYABIASHARA wadogo wa madini ya Tanzanite, wameishtaki Kampuni ya Tanzanite One kwa Kamati Maalumu ya Bunge inayochunguza biashara ya madini ya Tanzanite wakidai inawanyanyasa katika shughuli za uchimbaji wa madini.

Aidha, wameiomba Kamati kuwasilishi bungeni pendekezo la marekebisho ya sheria ili kubadili mfumo wa sasa wa uchimbaji, ili madini hayo yachimbwe kimshazari badala ya wima huku wakisistiza kwa kudai kuwa Tanzanite One imesababisha vifo na majeruhi ya wachimbaji wadogo katika eneo hilo la migodi.

Ombi la wafanyabishara hao limetolewa mbele ya Kamati hiyo inayoongozwa na Mwenyekiti, Dotto Bitego mara baada ya kutembelea machimbo. Kiongozi wa wachimbaji kutoka Gem & Rock Venture, Charles Mnyalu, aliwaeleza wajumbe wa Kamati kuwa licha ya kufanya kazi kwa miaka kumi, vurugu kati yao zimeanza baada ya migodi yao kuonesha dalili ya kupata madini.

Post a Comment

0 Comments