80% ya magonjwa Manispaa ya Kinondoni hutoka na uchafu- Meya Sitta

80% ya magonjwa Manispaa ya Kinondoni hutoka na uchafu- Meya Sitta




Wadau wa afya na Walimu wametakiwa kutoa elimu kwa wananfunzi na jamii kwa ujumla ,juu ya kunawa mikono kabla ya kula chakula ili kupunguza kasi ya magonjwa ya mlipuko.
Mstahiki meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni,akikata utepe katika uzinduzi wa Mradi wa Kuosha Mikono iliyofanyika leo jijini Dar es salaam.


Akizungumza mapema leo , Mstahiki Meya wa halmashauri ya Manispaa ya kinondoni, Benjamin Sitta katika uzinduzi wa mradi wa kuosha mikono, amesema mradi huo ni sehemu muhimu kwa wananfunzi na jamii kujenga tabia hiyo.


Amesema ili nchi iwe na maendeleo lazima watu wake wawe na afya,na ukosefu wa afya hulitia taifa hasara,lakini pia inapoteza muda mwingi wa kulitumikia taifa.


Aidha amesema ni vema watu wakaelewa kwamba ni asilimia 80%ya magonjwa yanayosababishwa na uchafu ikiwamo kipindupindu,tyfod,kichocho,homa ya tumbo.

Kupitia mradi huo JICA imejitolea kiasi cha shilingi milioni 53 kwa ajiri ya kuunga mkono katika kuendeleza mradi huo,ambapo lengo lake ni kueleimisha watoaji wa huduma ya afya,Wanafunzi na walimu wa shule ya msingi,katika kata ya kigogo,tandale,na magomeni na kuhusisha shule 15, vituo vya afya 05vilivyopo ndani ya kata hizo.

Mwakilishi kutoka ofisi ya JICA Bw. Kei Umetsu.


Mradi huo utaendeshwa kwa kufundisha wanafunzi 100 kwa vitendo kutoka katika shule zilizo tajwa,wahudumu wa afya 30 kutoka kwenye zahanati tano(Mburahati,kigogo,tandale, Moroviani na magomeni).

Post a Comment

0 Comments